Bozize kuongoza muungano wa vyama vya waasi CAR

François Bozize aongoza chama cha umoja wa waasi cha CPC katika Jamhuri ya Afrika ya Kati

1606115
Bozize kuongoza muungano wa vyama vya waasi CAR

Katika nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), kiongozi aliyeondolewa madarakani François Bozize ameripotiwa kuingia uongozi kwenye chama cha umoja wa waasi kiitwacho Patriots Coalition for Change (CPC).

Kulingana na taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari vya kitaifa, Msemaji wa CPC Serge Bozanga alitangaza kwamba walipokea majibu mazuri kwa pendekezo lililowasilishwa kwa Bozize kuongoza CPC, ambayo iliundwa na muungano wa vikundi 6 vya waasi.

Bozanga alisema kuwa Bozize ambaye ni mwanajeshi mwenye uzoefu, ataratibu hatua zote za kijeshi za CPC.

Muungano wa CPC, uliundwa kwa ushirikiano wa 3R (Mwamko Mpya, Mahitaji, Uimarishaji), Kitengo cha Amani cha Jamuhuri ya Afrika ya Kati (UPC), Jumuiya ya Wazalendo ya Jamuhuri ya Afrika ya Kati (MPC), Chama cha Wananchi cha Mwamko Mpya kwa Jamhuri ya Afrika ya Kati (FPRC) na makundi ya waasi wa Kikristo wa Anti-Balaka.

Baada ya Mahakama ya Katiba ya CAR kukataa kukubali ombi la kugombea kwa kiongozi aliyeondolewa madarakani Francois Bozize katika uchaguzi wa urais kwa kutokana na "jaribio la uhalifu na mauaji ya halaiki" na "kujumuishwa katika orodha ya vikwazo ya Umoja wa Mataifa", mapigano makali yalianza kati ya serikali na vikundi vya silaha mnamo tarehe 18 Desemba 2020.

Nchi hiyo ambayo takriban asilimia 80 inadhibitiwa na vikundi vya silaha, makundi ya waasi yaliyoko chini ya chama cha muungano wa wazalendo (CPC) yalianzisha harakati za kuuteka mji mkuu wa Bangui mnamo mwezi Desemba.

Serikali na UN zilimtuhumu Bozize, ambaye alitajwa kuwa mhusika wa mizozo hiyo na kudaiwa kutaka kundaa mapinduzi.Habari Zinazohusiana