Mlipuko wa bomu Mogadishu

Mlipuko umetokea mbele ya mgahawa wenye shughuli nyingi huko Mogadishu, mji mkuu wa Somalia

1596068
Mlipuko wa bomu Mogadishu

Mlipuko umetokea mbele ya mgahawa wenye shughuli nyingi huko Mogadishu, mji mkuu wa Somalia.

Mashuhuda wa mlipuko huo mbele ya mgahawa huo uitwao "Lul Yemeni" wilayani Hamar Jajab walisema kuwa waliona moshi mzito ukitokea eneo hilo.

Kwa mujibu wa habari, mgahawa huo ulikuwa karibu na Bandari ya Mogadishu na mpaka hivi sasa haijulikani bado endapo kuna majeruhi katika mlipuko huo ama la.

Mshambuliaji wa kujitoa mhanga alilipua bomu mbele ya mgahawa huo mnamo 2020, na kupelekea watu wengi kujeruhiwa.Habari Zinazohusiana