Wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu watekwa nyara na Boko Haram

Kundi la Boko Haram lashambulia ofisi za misaada ya kibinadamu na kuteka nyara wafanyakazi 7 nchini Nigeria

1594359
Wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu watekwa nyara na Boko Haram

Wafanyakazi 7 wa misaada ya kibinadamu wameripotiwa kutekwa nyara katika mashambulizi yaliyotekelezwa na shirika la kigaidi la Boko Haram kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Magaidi waliendesha mashambulizi ya silaha dhidi ya wanajeshi wilayani Dikwa katika jimbo la Borno.

Katika mashambulizi hayo, wafanyikazi 7 wa misaada ya kibinadamu wanaohudumu katika mkoa huo walitekwa nyara, huku ofisi za wafanyikazi wa misaada ya kibinadamu na hospitali zikichomwa moto na wanamgambo wa Boko Haram.

Edward Kallon, Mratibu wa Misaada ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini Nigeria, alilaani mashambulizi hayo na kuelezea wasiwasi wake juu ya usalama wa umma katika eneo hilo.

Kallon alisema kuwa takriban watu 100,000 wanaohitaji misaada ya kibinadamu katika eneo hilo wako hatarini kutokana na mashambulizi.

Kwa upande mwingine, watu 16 walipoteza maisha kwenye mashambulizi yaliyotekelezwa na watu wenye silaha katika jimbo la Kaduna.

Kamishina wa Usalama na Mambo ya Ndani wa Jimbo la Kaduna Samuel Aruwan, alibainisha kuwa watu wenye silaha wasiojulikana walishambulia vijiji vya mkoa wa Zangon Kataf na Kurmin Gandu.

Aruwan alitangaza kuwa watu 16 walipoteza maisha na wengine wengi walijeruhiwa katika mashambulizi hayo.

Akielezea kuwa nyumba 10 na pikipiki 2 ziliharibiwa katika mashambulizi hayo, Aruwan alisema wakazi wa mkoa huo waliacha nyumba zao kwa hofu ya usalama.

Aruwan pia aliripoti kuwa vikosi vya usalama vimetumwa katika eneo hilo na uchunguzi umeanzishwa juu ya tukio hilo.Habari Zinazohusiana