Marufuku ya safari za ndege Zamfara Nigeria

Rais Buhari atangaza marufuku ya safari za ndege katika jimbo la Zamfara nchini Nigeria

1594425
Marufuku ya safari za ndege Zamfara Nigeria

Jimbo la Zamfara la Nigeria limetangazwa kuwa eneo la ‘‘marufuku ya safari za ndege’’ kutokana na visa vya ghasia.

Rais Mohammed Buhari alikutana na Baraza la Usalama la Kitaifa kwenye makazi yake katika mji mkuu, kutokana na ghasia zilizotokea jimbo la Zamfara hivi karibuni.

Mshauri wa Usalama wa Kitaifa Babagana Monguno aliwaambia waandishi wa habari baada ya mkutano huo kwamba Rais Buhari ametangaza Zamfara kuwa eneo la "marufuku ya safari za ndege."

Akifahamisha kuwa Buhari pia alipiga marufuku shughuli za uchimbaji madini ya dhahabu katika eneo hilo, Monguno alisema kwamba ameamuru vikosi vya usalama vilivyotumwa kudumisha hali ya utulivu haraka iwezekanayo.

Monguno pia aliashiria kwamba maeneo yote yaliyoko chini ya udhibiti wa makundi ya silaha yatarudishwa na kusema,

"Hatuwezi kumudu vifo vya raia wakati wa kutekeleza operesheni dhidi ya makundi ya silaha. Hatutakuwa chini ya usaliti. Serikali ina jukumu la kuonyesha kuwa inawajali raia wake."

Watu wenye silaha walishambulia shule ya upili ya wasichana wilayani Jangebe katika jimbo la Zamfara mnamo Februari 26, na kuwateka nyara wanafunzi 317. Wanafunzi 279 kati ya waliotekwa waliokolewa hapo jana.

Hali ya Zamfara inashuhudia mapigano makali kati ya jamii ya Fulani, ambao wamekuwa wakifanya ufugaji kwa miaka 5, na makabila mengine ya kilimo.

Takriban watu elfu 2 walipoteza maisha kutokana na mizozo katika eneo hilo, na maelfu ya watu walilazimika kukimbia makazi yao.Habari Zinazohusiana