Uhaba wa chakula nchini Somalia

Janga la Covid-19 lazorotesha uchumi wa Somalia na kusababisha uhaba wa chakula kwa familia nyingi

1594251
Uhaba wa chakula nchini Somalia

Uchumi wa nchi ya Somalia umeathiriwa na janga la corona (Covid-19) na kusababisha uhaba wa chakula ambapo wananchi wanaishi kwa mlo mmoja tu kwa siku.

Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) iliripoti kuwa nchini Somalia, ambapo mlipuko wa janga la Covid-19 uliathiri vibaya uchumi wake, wananchi hula mlo mmoja tu kwa siku majumbani mwao.

Katika taarifa iliyotolewa kwenye akaunti ya Twitter ya OCHA, iliarifiwa,

"Uhaba wa chakula nchini Somalia unamaanisha kila familia inakula mlo mmoja kwa siku."

Taarifa hiyo pia ilisema kwamba, kufikia Agosti, takriban watoto 850,000 walio chini ya umri wa miaka 5 wanaweza kukabiliwa na utapiamlo.

Wakati watu milioni 1.3 wakilazimika kuhama makazi yao mwaka 2020 nchini humo, kuna mipango iliyopo inayolenga kutoa misaada ya kibinadamu kwa watu milioni 3.1 mwaka huu.

Kulingana na serikali ya Somalia na UN, dola bilioni 1 zinahitajika kwa shughuli za misaada ya kibinadamu nchini humo mwaka huu.Habari Zinazohusiana