Watu 35 wapoteza maisha katika mapigano Chad

Watu 35 wamepoteza maisha katika mapigano kati ya wachungaji wa kuhamahama na wakulima kusini mwa nchi ya Afrika ya Kati Chad

1586347
Watu 35 wapoteza maisha katika mapigano Chad

Watu 35 wamepoteza maisha katika mapigano kati ya wachungaji wa kuhamahama na wakulima kusini mwa nchi ya Afrika ya Kati Chad kutokana na shida ya malisho.

Afisa wa Wilaya ya Salamat Mara Maad aliripoti kuwa mapigano kati ya pande hizo mbili yalisababisha vifo vya watu 35, pamoja na askari mmoja.

Akibainisha kuwa mapigano hayo yalianza mnamo Februari 15, Maad alisema kuwa vikosi vya usalama vilitumwa kwa mkoa huo kuhakikisha utulivu.

Mnamo Novemba, watu 22 walipoteza maisha katika mzozo kama huo katika mkoa wa Kabbia kusini mwa nchi.

Kwa miaka mingi, mapigano yamekuwa yakitokea kati ya wakulima na wachungaji wa kuhamahama kusini mwa Chad kwa sababu ya shida ya malisho na kwamba mifugo huharibu shamba.Habari Zinazohusiana