Shambulizi la bomu Somalia

Mbunge wa zamani wa Somalia ajeruhiwa kwenye mlipuko wa bomu mjini Mogadishu

1569590
Shambulizi la bomu Somalia

Watu 5 wameripotiwa kupoteza maisha katika shambulizi la bomu lililotekelezwa kwenye gari la mbunge wa zamani Hasan Afrah katika mji mkuu wa Mogadishu nchini Somalia.

Kulingana na taarifa za habari zilizopatikana kutoka kwa vyanzo vya usalama, bomu lililowekwa barabarani lililipuka katika wilaya ya Shibis wakati gari la mbunge wa zamani  Afrah lilipokuwa likipita.

Kulingana na maelezo ya kwanza, watu 5 walifariki na wengine 3 walijeruhiwa ikiwa ni pamoja na Afrah.

Vikosi vya usalama vilitumwa kwenye eneo la tukio baada ya mlipuko.

Hakuna taarifa rasmi iliyotolewa na serikali kuhusu shambulizi hilo.

Hadi kufikia sasa hakuna yeyote aliyedai kuhusika na shambulizi.Habari Zinazohusiana