Barua kuhusu uchaguzi mkuu wa Libya kwa UN

Waziri Mkuu wa Libya Fayez al-Serraj atuma barua kwa UN kuhusu uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika

1569304
Barua kuhusu uchaguzi mkuu wa Libya kwa UN

Waziri Mkuu wa Libya Fayez al-Serraj alitoa wito kwa Umoja wa Mataifa (UN) na Baraza la Usalama  kuunga mkono masuala yote ya kufanya uchaguzi nchini humo.

Serraj alituma barua kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na kwa Mwakilishi wa Kudumu wa UN nchini Tunisia  Tariq al-Adab, ambaye pia ni mwenyekiti wa kikao cha Baraza la Usalama.

Barua hiyo iliyotumwa ilijumuisha ujumbe uliosoma, "Tunatarajia Umoja wa Mataifa utatuma timu haraka iwezekanavyo kutathmini mahitaji na kushauriana na kuratibu Baraza Kuu la Uchaguzi la Libya ili kufanikiwa mchakato huu muhimu wa kitaifa."

Serraj pia alihimiza Baraza la Usalama kupitisha azimio la uchaguzi mkuu na kupokea tarehe iliyoidhinishwa na wananchi wa Lbya na kutuma wajumbe wa Usaidizi wa Libya wa UN kutoa mwelekeo muhimu wa kufanikisha uchaguzi.

Uchaguzi mkuu uliamuliwa kufanywa Desemba 24 nchini humo, kufuatia "Mkutano wa Mazungumzo ya Kisiasa wa Libya", ambao ulifanyika chini ya uongozi wa UN, na watu 75 walichaguliwa kuwakilisha sehemu tofauti za kisiasa na kijamii nchini Libya.Habari Zinazohusiana