Utalii wa Chad kutambulishwa na Uturuki

Waturuki watatambulisha utalii wa Chad, moja ya nchi za Afrika, ulimwenguni.

1541987
Utalii wa Chad kutambulishwa na Uturuki

Waturuki watatambulisha  utalii wa Chad, moja ya nchi za Afrika, ulimwenguni.

Makubaliano yalitiwa saini kati ya Taasisi ya Jukwaa la Utalii Ulimwenguni na Wizara ya Utalii ya Chad kwa madhumuni ya kuandaa Jukwaa la Utalii Ulimwenguni huko Chad mnamo Machi, kukuza utalii wa Chad, kuongeza uwekezaji wa nchi katika eneo hili na idadi ya watalii.

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini iliyofanyika katika hoteli katika mji mkuu Ankara, Waziri wa Utalii na Utamaduni wa Chad Patalet Geo alisema kuwa makubaliano waliyosaini na Taasisi yapanua maono yao katika uwanja wa utalii.

Rais wa Taasisi ya Jukwaa la Utalii Ulimwenguni Bulut Bağcı alisisitiza kuwa utalii wa nchi hiyo ulikabidhiwa kwa Waturuki kwa kutia saini makubaliano na kusema,

"Tutaupa kipaumbele  utalii wa Chad na kufanya mapato ya nchi katika uwanja huu kuongezeka kwa kasi."


Tagi: #Chad , #utalii

Habari Zinazohusiana