Taha achaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa OIC

Husein Ibrahim Taha ndiye Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC)

1536201
Taha achaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa OIC

Mgombea wa Chad Husein Ibrahim Taha, amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC).

Katika mkutano wa 47 wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa OIC uliofanyika Niamey, mji mkuu wa Niger, shughuli ya upigaji kura iliendeshwa kwa ajili ya kumchagua mgombea atakayechukuwa nafasi ya Katibu Mkuu wa OIC Yusuf bin Ahmed al-Useymin, ambaye muda wake wa kuhudumu unamalizika Novemba 2021.

Mgombea wa Chad Husein Ibrahim Taha, alichaguliwa kwa kauli moja kuwa katibu mkuu wa 12 wa jumuiya hiyo.

Miongoni mwa wagombea wa nafasi ya Katibu Mkuu wa OIC walikuwa ni katibu mkuu wa sasa Useymin ambaye alijiondoa kwenye kinyang'anyiro, Benin na Nigeria nazo ziliamua kuunga mkono Chad.Habari Zinazohusiana