Vifo vyaongezeka Sudan

Idadi ya watu waliopoteza maisha katika janga la mafuriko nchini Sudan imeongezeka hadi 103.

1487949
Vifo vyaongezeka Sudan

Idadi ya watu waliopoteza maisha katika janga la mafuriko nchini Sudan imeongezeka hadi 103.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani, mtu mwingine amepoteza maisha  katika mafuriko  yaliyosababishwa na mvua kubwa kwa miezi kadhaa.

Kwa hivyo, idadi ya watu waliopoteza maisha imeongezeka hadi 103.

Watu 50 wamejeruhiwa kwa sababu ya mafuriko, nyumba 69,551 zimeharibiwa.

Wizara imetangaza kwamba zaidi ya ekari elfu 4 za ardhi ya kilimo zimeharibiwa kutokana na mvua kubwa katika majimbo 16 kati ya 18, na zaidi ya ng'ombe elfu 5 wameangamia.

Uwakilishi wa Kudumu wa Sudan kwa Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa mashirika ya kimataifa kuisaidia nchi hiyo ambayo imeharibiwa vibaya na mafuriko.

Wizara ya Umwagiliaji na Rasilimali za Maji imetangaza kuwa kiwango cha maji ya Mto Nile kimeongezeka zaidi katika karne iliyopita na kilikaribia mita 18.

Baraza la Ulinzi na Usalama la Sudan limetangaza dharura kwa miezi 3 kutokana na janga la mafuriko.Habari Zinazohusiana