Watoto kumi wauawa kwa radi Uganda

Takriban watoto 10 wamepigwa na kuuawa na radi wakati wa mvua kubwa kaskazini magharibi mwa Uganda.

1481009
Watoto kumi wauawa kwa radi Uganda

Takriban watoto 10 wamepigwa na kuuawa na radi wakati wa mvua kubwa kaskazini magharibi mwa Uganda.

Kulingana na shirika la habari la APA,tukio hilo limetokea wakati watoto tisa kati ya 10 wenye umri wa miaka 13-15 walipokuwa wakijikinga na mvua kwenye kibanda baada ya kupumzika kutoka kwenye mechi ya mpira wa miguu.

Mtoto mmoja kati ya 10 waliofariki, ameripotiwa kufia njiani wakati alipokuwa akipelekwa hospitalini.

Matukio hayo mawili yametokea katika mji wa Arua.

Katika wiki za hivi karibuni, Uganda imeshuhudia dhoruba nzito za radi.

Mnamo mwaka wa 2011, Uganda ilishuhudia tukio kama hilo ambapo watoto 18 walipigwa na radi na kuuawa katika eneo la magharibi mwa nchi hiyo.Habari Zinazohusiana