Niger yaathiriwa vibaya na mafuriko

Watu 45 wameripotiwa kufariki kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa

1480695
Niger yaathiriwa vibaya na mafuriko

Watu 45 wameripotiwa kufariki kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa ambazo zimekuwa zikinyesha tangu mwezi Juni nchini Niger.

Katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Kitengo cha Masuala ya Kibinadamu na Usimamizi wa Maafa nchini Niger, imeelezwa kuwa watu 45 wamepoteza maisha na zaidi ya watu 226,000 wameathiriwa kwa kiasi kikubwa na mafuriko hayo.

Majengo ya nyumba 20,000, na misikiti 24 yamefunikwa na maji.

Mafuriko hayo yameathiri pia maelfu ya mifugo na mazao.

Karibu nusu ya watu nchini Niger wanaishi karibu na mto Niger katika mji mkuu wa Niamey, ambapo nyumba nyingi zimeathiriwa na mafuriko tangu mwanzo mwa wiki.

Vilevile nyumba nyingi ziko kwenye ukingo wa mto, jambo linaloongeza hali ya hatari ya wakazi wa maeneo hayo.

Mwaka jana watu 32 walipoteza maisha katika janga la mafuriko nchini humo.Habari Zinazohusiana