Shambulizi dhidi ya wanajeshi Somalia

Askari 3 wamepoteza maisha katika shambulizi la bomu na silaha kwenye uwanja wa jeshi kusini mwa Somalia

1474530
Shambulizi dhidi ya wanajeshi Somalia

Askari 3 wamepoteza maisha katika shambulizi la bomu na silaha kwenye uwanja wa jeshi kusini mwa Somalia.

Msemaji wa serikali Ismail Muhtar Omer ameripoti kwamba wanamgambo wa kundi la kigaidi la Al-Shabab wameshambulia kituo cha jeshi na gari lililokuwa limetegwa bomu katika eneo la Bay.

Ömer amesema kuwa baada ya mlipuko huo kulikuwa na mzozo kati ya askari na wanamgambo na shambulizi kuanza tena.

Adan Kheyrow, mmoja wa maafisa wa jeshi katika eneo la Bay amesema kwamba askari 3 wameuawa katika mapigano hayo.

Wanamgambo wengi wa al-Shabaab nao wameuawa katika ghasia hizo.Habari Zinazohusiana