Watu 12 wauawa katika shambulizi Nigeria

Watu 12 wamepoteza maisha katika shambulizi la silaha katikati mwa Nigeria.

1468442
Watu 12 wauawa katika shambulizi Nigeria

Watu 12 wamepoteza maisha katika shambulizi la silaha katikati mwa Nigeria.

Kulingana na ripoti ya vyombo vya habari vya kitaifa, watu wenye silaha, ambao hawajatambuliwa mpaka sasa wameshambulia kwa silaha eneo la Kogi nchini humo.

Watu 12 wamefariki katika shambulizi hilo, watu wengi wamejeruhiwa.

Kwa upande wake, Msemaji wa Wizara ya Ulinzi John Enenche amesema kwamba ameanzisha operesheni dhidi genge la silaha katika jimbo la Bayelsa.

Enenche alibaini kuwa wanachama 6 wa genge hilo wameangamizwa wakati wa operesheni hiyo na silaha kukamatwa.

 Habari Zinazohusiana