Afrika Magharibi yabadlisha sarafu

Nchi zaanza kutumia Eco

1426503
Afrika Magharibi yabadlisha sarafu

Ni rasmi kwamba Eco itachukua nafasi ya CFA Franc kama sarafu mpya kwa nchi nane za Francophone ambazo zinaunda Jumuiya ya Uchumi na Fedha ya Afrika Magharibi (UEMOA).

Baraza la Mawaziri la Ufaransa lilipitisha rasmi muswada mapema mwezi huu ambao uliboresha marekebisho ya makubaliano ya kifedha ambayo yataiunganisha serikali ya Ufaransa na nchi nane za Afrika.

Kufanya hivyo kumeleta tamati miaka 75 ya kutawaliwa kwa baadhi ya nchi za Africa na Jamhuri ya Ufaransa ambayo ilizilazimisha nchi hizo kuweka kuweka amana - akiba yao ya fedha za kigeni katika Banque de France, inayojulikana kama Hazina ya Ufaransa.


Benin, Burkina Faso, Guinea-Bissau,Ivory Coast, Mali, Niger, Senegal na Togo sasa watahifadhi akiba yao ndani ya Benki Kuu ya Afrika Magharibi, au BCEAO.

Eco itakuwa na kiwango cha kubadilishana cha 655.957 euro.

CFA franc, au Communute d'Afrique, imekuwa ikitumika tangu 1945 na iliundwa kwa sababu ya udhaifu wa Franc baada ya Vita vya pili vya dunia.


Ingawa limekuwa ni lengo la Afrika Magharibi kwa miongo kadhaa kupitisha sarafu yao wenyewe mnamo Julai 1 mwaka jana nchi wanachama wa UEMOA zilitangaza nia yao ya kuacha kutumia CFA na kuanza kutumia Eco.
 

Eco inatarajiwa kupitishwa na nchi wanachama mnamo Julai 1.

Serikali ya Ufaransa pia itaondoa uwepo wake kutoka uongozi wa Afrika Magharibi iliyokuwa ikihusiana nao kama vile BCEAO.

Baraza la Mawaziri lilionyesha jukumu lao katika suala hilo na kusema kuwa,

"Nafasi hii mpya inatuwezesha kuunga mkono UEMOA katika kujitolea kwake kutekeleza mradi huo wa sarafu ya Jumuiya ya Uchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS)," .

Nchi zingine sita za Afrika ya Kati ambazo ni za Jumuiya ya Uchumi na Fedha ya Afrika ya Kati (CAEMU) zinatumia CFA, ikiwemo Jamhuri ya Afrika ya Kati, Cameroon, Gabon, Guinea ya Ikweta na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
 Habari Zinazohusiana