Watu zaidi ya  100 wamefariki katika  mapigano ya kikabila nchini Sudan Kusini

Watu zaidi  ya  100 wameripotiwa kuuawa katika mapigano ya kikabila yaliotokea nchini humo  katika eneo lake la Kaskazini-Mashariki

1421775
Watu zaidi ya  100 wamefariki katika  mapigano ya kikabila nchini Sudan Kusini


Watu zaidi  ya  100 wameripotiwa kuuawa katika mapigano ya kikabila yaliotokea nchini humo  katika eneo lake la Kaskazini-Mashariki.

Nchini Sudani Kusini, mapigano hayo ya kikabila yameripotiwa kutokea katika siku 5 zilizopita  na kupelekea maafa hayo.

Mapigano ya kikabila yaliotokea nchini Sudani Kusini yamepeleka kuuawa kwa watu zaidi ya  100 wakiwemo wafanyakazi watano wa mashirika  yasiokuwa ya serikali.

Mratibu wa shirika  mmoja la Umoja wa Mataifa  nchini Sudani Kusini , Alain Noudehou  amefahamisha katika taarifa ya kwamba  UM unalaani vikali mashambuliz hayo katika taifa changa barani Afrika ikiwa ni ukingo mkubwa katika zjitihada za kutafuta amani  ya kuudumu na maendelea nchini humo.

Wafanyakazi watatu wa Umoja wa Mataifa wameirpotiwa kuuawa katika mkoa wa Jonglei.

Mratibu huyo ametoa wito wa kusitishwa haraka  ghasia katika eneo hilo.

Alain Noudehou amesema, watu zaidi ya  100 wameuawa  katika mapigano ya kikabila yaliotokea  nchini Sudani Kusini tangu Mei  16.Habari Zinazohusiana