Mwanamuziki mashuhuri Mory Kante afariki dunia

Mwanamuziki mashuhuri nchini Guinea Mory Kante amefariki akiwa na umri wa miaka 70.

1422104
Mwanamuziki mashuhuri Mory Kante afariki dunia

Mwanamuziki mashuhuri nchini Guinea Mory Kante amefariki akiwa na umri wa miaka 70.

Kulingana na ripoti katika vyombo vya habari vya kitaifa, Kante amepoteza maisha akiwa hospitalini alipotibiwa katika mji mkuu wa Guinea, Konakri.

Kante, ambaye alizaliwa mnamo Machi 29, 1950 katika mji wa Kissidougou, alipata umaarufu ulimwenguni kote na wimbo "Ye ke ye ke" aliouimba mnamo 1977.

Mory Kante ni mwimbaji wa Kiafrika, ambaye albamu yake imefikia idadi kubwa zaidi ya mauzo hadi sasa.Habari Zinazohusiana