Uturuki yalaani shambulizi la kigaidi Niger

Uturuki imelaani shambulizi la kigaidi nchini Niger.

1420903
Uturuki yalaani shambulizi la kigaidi Niger

Uturuki imelaani shambulizi la kigaidi nchini Niger.

Wizara ya mambo ya nje ya Uturuki imetuma salamu za rambirambi Niger na kuwatakia wale wote waliopoteza maisha katika shambulizi hilo kulala mahai pema peponi.

"Katika taarifa iliyoandikwa kutoka Wizara ya Mambo ya nje, imebainika na huzuni kubwa kuwa kuna askari waliokufa na kujeruhiwa katika shambulizi la kigaidi huko Diffa, Niger siku ya Jumatatu."

"Tunalaani shambulizi hilo la kigaidi. Tunawaombea rehema ya Mungu na kuwatakia ahueni wale wote waliojeruhiwa na kutoa pole ya dhati kwa watu wa Niger na serikali yote kwa ujumla.",ilisema taarifa hiyo.

Imeripotiwa kuwa askari 12 waliuawa na 10 kujeruhiwa katika shambulizi lililotekelezwa na kundi la kigaidi la Boko Haram huko Niger kwenye Kituo cha Jeshi la Blabrine katika mji wa Diffa Jumatatu usiku.Habari Zinazohusiana