Rais Kagame amfuta kazi waziri wa afya kufuatia kudanganya kuhusu Corona

Rais Paul Kagame amemfuta kazi waziri wa afya wa nchi hiyo Dkt Gashumba kwa tuhuma kwamba waziri huyo alimdanganya juu ya uwepo wa vifaa tiba vya kupima virusi vya Corona, Covid-19

1366368
Rais Kagame amfuta kazi waziri wa afya kufuatia kudanganya kuhusu Corona

Rais Paul Kagame wa Rwanda amfuta kazi waziri wa afya wa nchi hiyo Dkt Gashumba kwa madai kwamba waziri hyo alimdanganya juu ya uwepo wa vifaa tiba kwa ajili ya kupima virusi vya Corona, Covid-19.

Akizungumza katika mkutano wa kitaifa wa viongozi kujitathimini, Rais Paul Kagame alisema,

“Asubuhi moja nilimpigia simu kiongozi mmoja pamoja na waziri mkuu kuzungumzia kuhusu virusi vya Corona, nikawaambia watuchunguze sote kabla ya mkutano huu wa viongozi. Nikawaambia wamwambie waziri wa afya ahakikishe hilo linafanyika.”

“Akajibu tuna vifaa tiba vya kupima Corona vipatavyo 3,500 na kwamba tukitumia 400 kwa ajili ya kupima viongozi, tutakuwa tumevipunguza sana vifaa tiba tulivyonavyo. Mtu niliyemtuma akamwambia kwamba hayo ni maagizo na kama anapingamizi anipigie mimi”

“Baadae tukajakutambua kwamba hatuna vifaa tiba idadi aliyoitaja waziri.

Tuna vifaa tiba 95 tu na sio 3500 kama alivyosema waziri, nilivyomuuliza kuhusu hilo akaanza kurefusha maneno kwa kujitetea.

Nyie viongozi hamuwezi hata kusema ukweli, mtawazaje kutatua matatizo ?” alisema Kagame.Habari Zinazohusiana