Watu 100 kutoka China watengwa kiafya nchini Uganda

Wasafiri zaidi ya 100 kutoka China watengwa baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege mjini Kampala  kutokea nchini China

Watu 100 kutoka China watengwa kiafya nchini Uganda


Wasafiri zaidi ya 100 kutoka China watengwa baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege mjini Kampala  kutokea nchini China.

Mamlaka ya uwanja wa ndege huo nchini Uganda umefahamisha kuwa uamuzi huo umechukuliwa kutokana na virusi vya corona kuathiri binadamu na kusababisha maada kwa muda mfupi kwa mtu alieambukiwa.

Mwishoni mwa mwaka  2019, China ilitangaza kugundua virusi vipya vya corona aina ya nCoV katika jimbo la Wuhan.

Ulimwengu mzima ulichukuwa tahadhari na kuanza mikakati ya kukabiliana na maambukizi mapya ya virusi hivyo.

Waziri wa afya wa Uganda Dr. Jane Aceng  amezungumza na wanahabari na kuwafahamisha kuwa  watu 100 kutoka nchini China wametengwa kiafya  na wasalia katika uchunguzi wa kiafya kwa muda wa  siku 14 katika hospitali tofauti.
Waziri wa afya huyo amesema kwamba miongoni mwa watu waliotengwa wamo raia 44 wa China.

Kwa uapnde mwingine, raia mmoja wa Argentina na mwengine wa China wametengwa kwa ajili ya uchunguzi wa afya nchini Gana.


 Habari Zinazohusiana