Urithi aliouacha Mugabe wawa gumzo

Urithi ulioachwa na Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe wawa gumzo

Urithi aliouacha Mugabe wawa gumzo

Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe, alifayefariki dunia mnamo Septemba 6 ameacha urithi wa mamilioni ya dola imefahamika.

Katika habari iliyochapishwa na gazeti la The Herald limeandika kwamba utajiri wa Mugabe ambao kwa miaka mingi ulizua mjadala katika nchi hiyo,imefahamika kwamba ameacha dola milioni 10 katika benki moja ya nchini humo, Katika mji mkuu wa nchi hiyo, Harare ameacha nyumba 4, magari 10 na shamba lenye ukubwa wa hekari 11.

Habari hiyo ilitayarishwa kutokana na orodha iliyowasilisha mahakama kuu mnamo mwezi Oktoba na binti wa Mugabe, Bona Chikowere.

Chikowere aliitaka mahakama isajili mali na fedha zote za Mugabe kwa jina la familia. Habari hiyo pia ilisema kwamba Mugabe hakuacha wosia wowote.

Inasemekana kwamba kabla ya kifo chake ndani na njeya nchi, Mugabe alikuwa na jumla ya  utajiri wa dola milioni 100.Habari Zinazohusiana