Ndege ya abiria yashambuliwa kwa silaha nchini Cameroun

Ndege ya abiria yashambuliwa kwa silaha wakati ikitua huko nchini Cameroun

Ndege ya abiria yashambuliwa kwa silaha nchini Cameroun

Imeelezwa kwamba shambulizi la silaha limefanywa dhidi ya ndege ya abiria katika eneo la Cameroun inapozungumzwa lugha ya Kiingereza (Anglofon).

Shirika la ndege la Cameroun, Camair-Co limetoa taarifa ya maandishi isemayo kwamba ndege ya abiria yenye usajili TJ-QDP aina MA60  iliyokuwa ikitoka mji wa kibiashara doula kuelekea mji wa Bamenda uliopo katika eneo linapozungumzwa lugha ya kiingereza ilishambuliwa kwa silaha wakati ikitua.

Taarifa hiyo iliendelea kueleza kwamba rubani wa ndege hiyo alifanikiwa kuiongoza ndege hiyo kwa umahiri hata baada ya mashambulizi,hivyo hakuna mtu aliyepoteza maisha.

Moaka sasa haijawekwa wazi nani anahusika na shambulizi hilo.

 Habari Zinazohusiana