Mabadiliko ya tabia nchi yatishia bara la Afrika

Athari zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi zimeonekana kuliathiri zaidi bara la Afrika

Mabadiliko ya tabia nchi yatishia bara la Afrika

Shirika lisilokuwa la kiserikali “Save the Children”, limesema kwamba kutokana na mabadiliko ya tabia nchi duniani watu zaidi ya milioni 33 mashariki na kusini mwa Afrika hawana usalama wa chakula.

Shirika hilo limetoa taarifa ya maandishi isemayo kwamba majanga ya asili yameonyesha kuongezeka katika nchini kama Msumbiji, Somalia, Kenya, Sudan, Malawi, Ethiopia na Zimbabwe. kwa mwaka huu pekee zaidi ya watu 1200 wamepoteza maisha kutokana na mafuriko,maporomoko ya ardhi, vimbunga n.k.

Taarifa hiyo pia ilieleza kwamba joto kusini mwa Afrika limeongezeka mara 2 ukilinganisha na wastani wa joto la dunia.Kuanzia mwezi Juni 2019 zaidi ya watu milioni 7 katika mataifa 7 wamelazimika kuyahama makazi yao kutokana na mabadilko ya tabia nchi.

 Taarifa hiyo pia ilieleza kwamba zaidi ya watu milioni 33 katika mataifa ya Sudan kusini, Zimbabwe, Sudan, Somali, Zambiya, Ethiopia, Malawi, Kenya, Msumbiji na Madascar wanakabiliana na hali mbaya sana ya kukosa chakula, taarifa hiyo pia ilionya kwamba hali itaendelea kuwa mbaya zaidi.

Save the Children, ilitoa wito kwa viongozi walioshiriki warsha ya mabadiliko ya tabia nchi kuchukua hatua kubwa zaidi katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi.Habari Zinazohusiana