Moise Katumbi arejea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Moise Katumbi arejea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya kuishi uhamishoni mwa muda wa miaka mitatu

Moise Katumbi arejea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Mpinzani ambae alikuwa mshirika wa karibu wa rais  Joseph Kabila, Moise Katumbi  arejea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya kuishi uhamishoni kwa muda wa miaka mitatu.

Moise Katumbi amewasili katika uwanja wa ndege wa mjini Lubumbashi  mapema Jumatatu Mei 20  katika ndege yake binafsi.

Mpinzani huyo ambae alizuiliwa kushiriki katika uchaguzi mkuu uliofanyika JK Kongo amepokelewa kwa shangwe na wafuasia wake.

Katumbi ametoa shukrani kwa utawala wa rais Felix Tshisekedi kwa  kumruhusu kurejea nchini na kumpa haki yake  ya milimiki  hati ya kusafiria ambayo alikuwa amezuiliwa na utawala wa rais Joseph Kabila.Habari Zinazohusiana