Mtoto mdogo apona virusi vya Ebola JK Kongo

Mtoto mdogo  mwenye umri wa siku 42 apona Ebalo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Mtoto mdogo apona virusi vya Ebola JK Kongo

Mtoto mdogo mwenye umri wa siku 42 aripotiwa kupona Ebola huku mamae akiripotiwa kufariki Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mtoto huyo wa kike ambae alipewa jina la Danielle  alilazwa hospitali pamoja na mamae Aprili 11 mwaka 2019 kipindi ambacho alikuwa na siku 12.

Mtoto huyo amepona  virusi hivyo katika eneo la Masshariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, eneo ambalo  watu zaidi ya 1117 wamekwishafariki tangu kuibuka kwake  kwa mara nyingine  Agosti  mosi mwaka 2018.

Mtoto huyo ameruhiwa kuondoka katika kituo cha afya alipokuwa akipewa matibabu CTE Katwa katika mkoa wa Kivu Kusini.

Taarifa hiyo imethibitishwa na  wizara ya afya ya JK Kongo  Jumapili jioni kupitia kituo cha hhabari cha Uturuki Anadolu.

Daniella alikutwa na virusi hivyo baada ya kufanyiwa vipimo Aprili 12 na baada ya siku 30 alipopimwa kwa mara nyingine alikutwa salama na hana virusi hivyo.
Shirika la afya la Umoja wa Mataifa   limekwishwa  toa ruhusa ya  chanjo  dhidi ya  virusi vya ebola  huku shirika la Janssen Pharmaceutica  likisubiri  ruhusa kutoka  katika serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.


Tagi: JK Kongo , Ebola

Habari Zinazohusiana