Trump aliwashawishi MBS na Al Sisi kumsaidia Haftar

Jarida la American Wall Street limeandika kwamba Rais Trump aliwashawishi MBS na Al Sisi kumsaidia jenerali Haftar

Trump aliwashawishi MBS na Al Sisi kumsaidia Haftar

Inasemekana kwamba Rais wa Marekani , Donald Trump aliwashawishi mrithi wa kiti cha enzi mwana mfalme  wa Saudia, Muhammed bin Selman (MBS) pamoja na Rais wa Misri Abdulfattah al-Sisi kumsaidia jenerali Halife Haftar ambaye anapambana na vikosi vya serikali ya Libya inayotambuliwa wa Umoja wa Mataifa ili kuikamata Tripoli.

Habari iliyochapishwa na jarida la Amerikan Wall Street Journal ambapo chanzo chake ilikuwa ni kiongozi mmoja wa Marekani na wawili wa Saudia ilisema kulikuwa na majadiliano kuhusu Libya baina ya Trump, MBS na Al Sisi.

April 9 Rais  Trump alikutana na  Al Sisi Ikulu ya Marekani na  kwamwagiza amsaidie Jenerali Haftar .Baada ya mazungumzo hayo chanzo cha habari kinadokeza kwamba siku hiyo hiyo Trump alimpigia simu MBS na kumpa maagizo yale yale ya kumsaidia jenerali Hafter.

 Habari Zinazohusiana