Ukuta wa kanisa waanguka na kusababisha vifo DRC

Watu watano kutoka familia moja wamepoteza maisha yao baada ya ukuta wa kanisa kuanguka

Ukuta wa kanisa waanguka na kusababisha vifo DRC

Watu watano kutoka familia moja wamepoteza maisha yao wakati ukuta wa kanisa la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ulipoangukia nyumba katika jimbo la Kusini mwa Kivu.

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, ukuta wa kanisa katika kijiji cha Bagira, katika mji wa mashariki mwa Bukavu, uliharibiwa na mvua kubwa na kuangukia nyumba iliyo karibu nayo.

Watoto 3 ,baba yao na shangazi yao wamepoteza maisha baada ya kuangukiwa na kufunikwa na ukuta huo.

Inasemekana kuwa mama mtu alikuwa katika wodi ya kujifungua wakati wa tukio hilo.

DRC imendamwa na mvua kali za kitropiki kwa sasa.Mvua hizo husababisha uharibifu mkubwa nchini humo.

 

 


Tagi: mvua , ukuta , kanisa , vifo , DRC

Habari Zinazohusiana