Mashambulizi ya silaha nchini Mali: 4 wapoteza maisha

Watu wenye silaha washambulia na kusababisha vifo vya raia 4 nchini Mali

Mashambulizi ya silaha nchini Mali: 4 wapoteza maisha

Raia 4 wapoteza maisha baada ya kushambuliwa na watu wenye silaha eneo la Mopti katikati mwa nchi ya Mali.

Kwa mujibu wa habari za vyombo vya nchini humo, watu wenye silaha waliwashambulia raia waliokuwa wakitoka katika kijiji chaBandiagara kuelekea Tegrou, na kisha kutokomea kusikojulikana.

Katika tukio hilo  raia 4 walipoteza maisha na wengine 2 kujeruhiwa.


Tagi: Mali , Mopti

Habari Zinazohusiana