Mateka waokolewa nchini Nigeria

Mateka 27 miongoni mwao wakiwamo raia wa kigeni 5 waliokuwa wakishikiliwa na makundi yenye silaha waokolewa katika oparesheni maalum iliyofanywa na polisi

Mateka waokolewa nchini Nigeria

 

Mateka 27 waliokuwa wakishikiliwa na makundi yenye silaha nchini Nigeria waokolewa.

Akizungumza kwa niaba ya polisi wa jimbo la Kaduna, Muhammed Adamu,alisema oparesheni maalumu dhidi ya makundi ya kisilaha ziliendeshwa Kaduna na /zamfara.

Adamu alisema katika opareshehi hizo walifanikiwa kuwaokoa mateka 22 katika eneo la Birnin Gwari lililopo Kaduna na Zamfara waliokoa mateka 5 ambao walikuwa ni raia wa kigeni.

Katika oparesheni hiyo wanachama 2 wa kundi la watekaji waliuawa huku watu wengi wakitiwa nguvuni.

Oparesheni zilizoendeshwa katika jimbo la Kaduna katika wiki iliyopita zilipelekea watu 270 kukamatwa .


Tagi: Nigeria , Mateka

Habari Zinazohusiana