Ukame wapelekea hali ya dharura nchini Angola

Watu milioni 2.3 wanahitaji misaada ya chakula cha dharura kutokana na ukame nchini Angola.

Ukame wapelekea hali ya dharura nchini Angola

Watu milioni 2.3 wanahitaji misaada ya chakula cha dharura kutokana na ukame nchini Angola.

Kulingana na ripoti ya vyombo vya habari vya taifa hilo, ukameumeathiri maeneo ya kusini huku ardhi ya kilimo ikiwa imeathirika zaidi.

Imeelezwa kuwa ukame unasababisha mgogoro wa chakula na watu milioni 2.3 wanahitaji misaada ya chakula cha dharura.

Katika ripoti iliyochapishwa na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Watoto (UNICEF), mvua imekuwa tatizo kubwa nchini Angola.

Ripoti hiyo imeonyesha kwamba maelfu ya watoto wamepatiwa na utapiamlo kwa sababu ya ukame.

Mnamo mwezi Januari Rais wa Angola Joao Lourenço alitangaza hali ya dharura nchini na kusema kuwa umma unahitaji msaada wa haraka wa chakula.


Tagi: Angola , njaa , ukame

Habari Zinazohusiana