Afrika kusini kuwapa kipaumbele waislamu kipindi cha uchaguzi

Tume ya uchaguzi nchini Afrika kusini imesema kutokana na kwamba uchaguzi mkuu wa rais umeangukia katika mwezi wa Ramadhan, waislamu watapewa kipaumbele ili kuwarahisishia ibada hiyo

Afrika kusini kuwapa kipaumbele waislamu kipindi cha uchaguzi

Tume ya uchaguzi ya Afrika kusini imefahamisha kwamba imeweka urahisi kwa waislamu kupiga kura kutokana na uchaguzi kuangukua mwezi wa Ramadhan.

Kate Bapela kutoka tume ya uchaguzi ya Afrika kusini ametoa taarifa kwamba Kutokana na kwamba waislamu wanakuwa wamefunga katika mwezi wa Ramadhan, watapewa haki ya kipekee katika kupiga kura.

Bapela alisema uamuzi huo umechukuliwa ili kuwarahishia waislamu kufanya ibada yao.

Tangu kumalizaka kwa siasa za ubaguzi wa rangi nchini Afrika kusini mwaka 1994, huu utakuwa uchaguzi mkuu wa 6 wa rais. Nchi hiyo yenye idadi ya watu wapatao milioni 56, asilimia 2 ya watu wake ni waislamu.Habari Zinazohusiana