Ramadhani ya 7 rais wa zamani wa Misri akiwa kifungoni

Rais wa zamani aliechaguliwa chini ya misingi ya kidemokrasia afunga  Ramadhani yake ya 7 akiwa kifungoni

Ramadhani ya 7 rais wa zamani wa Misri akiwa kifungoni

Mohammed Morsi, rais wa zamani wa Misri aliechaguliwa chini ya misingi ya kidemokrasia  afunga Ramadhani yake ya 7 akiwa kifungoni.

Rais Mohammed Morsi aliondolewa madarakani kwa kupinduliwa mwaka 2013.

Ujumbe  wa maandishi uliotolewa na wanafamilia ya Morsi ameafahamisha kuwa Morsi amefungiwa katika chumba cha pekee na hana haki ya kutembelewa na watu wake wa karibu.

Morsi alikamatwa na kutupwa gerezani kinyume cha sheria ujumbe huo uliendelea kufahamisha.

Ni Rmadhani ya 7 Mohammed Morsi akiidiriki akiwa kifungoni.

Mtoto wa Morsi , Usame Morsi nae alitupwa gerezani katika chumba cha pekee ikiwa ni Ramadhani ya tatu kwa kumtetea baba yake  kikatiba.

Wanafamilia   wa Mohammed Morsi wamepatwa na wasiwasi kuhusu  afya yake  tangu alipofungiwa katika chumba cha pekee na kuwekewa marufuku ya kuonana na yeyote yule.

Wito  umetolewa kwa jumuiya ya kimataifa na mashirika ya  kutetea haki  za binadamu hususan Umoja wa Mataifa kufuatilia suala zima kuhusu kifungo cha Morsi.

Mohamed Morsi alichaguliwa kuwa rais Misri mwaka 2012 mwaka mmoja baada ya maandamano yaliopelekea rais Mubarak kuondoka madarakani.

Mwaka mmoja baadae Morsi alipinduliwa na jeshi Julia 3 mwaka 2013.Habari Zinazohusiana