Omar Al Bashir ahamishiwa gerezani

Kiongozi aliyepinduliwa nchini Sudan Omar Al Bashir ahamishiwa gerezani mjini Khartoum

Omar Al Bashir ahamishiwa gerezani

Kiongozi aliyepinduliwa nchini Sudan, Omar Al Bashir amehamishiwa katika gereza la Kober la mjini Khartoum.

Gazeti la "Ahir Lahza" limeripoti kwamba chanzo makini kutoka jeshini kimearifu kwamba Bashir Al Asad alihamishwa hapo jana kutoka katika makazi yake alipokuwa akishikiliwa na kupelekwa katika gereza kuu la  Kuber.

Bashir alikuwa akishikiliwa chini ya ulinzi mkali katika makaazi ya rais baada ya kuondolewa kwake madarakani na jeshi Aprili 11.Wakati huohuo waandamanaji bado wanaendelea kupiga kambi nje ya makao makuu ya jeshi wakitowa mwito wa kuundwa serikali ya kiraia na jeshi kujayakabidhi madaraka kwa amani.Habari Zinazohusiana