Wafanyakazi 8 wapoteza maisha kutokana na njaa nchini Mali

Wafanyakazi nane wa kampuni ya reli wameripotiwa kupoteza maisha nchini Mali.

Wafanyakazi 8 wapoteza maisha kutokana na njaa nchini Mali

Wafanyakazi nane wa kampuni ya reli wameripotiwa kupoteza maisha nchini Mali.

Kwa mujibu wa habari,wafanyakazi hao nane ni kati ya wafanyakazi wengi ambao wamefanya mgomo wa kutokula kwa muda wa miezi minne sasa kutokana na kutolipwa mishahara yao toka mwezi Mei mwaka jana.

Kulingana na ripot hiyo,wafanyakazi wengine wengi wapo mahospitalini kutokana na hali mbaya ya kiafya iliyosababishwa na mgomo huo.

Wafanyakazi hao walianza kugoma toka 18 Desemba 2018 wakidai kulipwa kwa mishahara yao.

Kwa upande mwingine,vyama vya waalimu vimetangaza kuendelea kugoma mpaka 17 Mei.

Walimu wanadai huduma rahisi za nyumba na kusaidiwa na serikali.


Tagi: reli , walimu , mishahara , vifo , njaa , mgomo , Mali

Habari Zinazohusiana