Shambulizi la silaha lapelekea vifo vya watu 15 Nigeria

Watu 15 wameuawa na watu 14 kujeruhiwa katika mashambulizi ya silaha katika maeneo ya Magharibi mwa Nasarawa, Nigeria.

Shambulizi la silaha lapelekea vifo vya watu 15 Nigeria

Watu 15 wameuawa na watu 14 kujeruhiwa katika mashambulizi ya silaha katika maeneo ya Magharibi mwa Nasarawa, Nigeria.

Msemaji wa Polisi wa Jimbo la Nasarawa Umar Shehu Nadada, amewaambia waandishi wa habari, watu wasiojulikana wamfanya shambulizi hilo katika kijiji cha Numa.

Nadada amesema kuwa wanaume wenye silaha walishambulia na kusababisha vifo vya 15 huku wengine 14 wakiwa wamejeruhiwa.

Msemaji huyo wa polisi amesema kuwa majeruhi wamefikishwa hospitali huku uchunguzi zaidi ukiwa unafanyika kuhusiana na shambulizi hilo Nasarawa.

Kutokana na mashambulizi ya hivi karibuni ya silaha nchini, serikali imezindua operesheni dhidi ya silaha katika mikoa ya Zamfara, Kebbi, Katsina, Niger na Sokoto.
 Habari Zinazohusiana