147 wafariki katika mapigano yanayoendelea Libya

Shirika la Afya duniani limeripoti kwamba watu wapatao 147 wamefariki na wengine 614 kujeruhiwa ndani ya siku 11 za mapigano yanayoendelea nchini libya

147 wafariki katika mapigano yanayoendelea Libya

 

Idadi ya vifo vilivyotokana na mapigano yanayoendelea nchini Libya yaliyodumu kwa muda wa siku 11 imefikia 147.

Shirika la afya duniani WHO kupitia kurasa zake za mitandao ya jamii imetoa taarifa kwamba  tangu yaanze mapigano ya mwisho  nchini Libya mpaka hivi sasa idadi ya vifo imefikia 147 huku majeruhi wakiwa 614.

Katika taarifa hiyo WHO imesema itatuma vifaa tiba na wataalamu wa afya nchini humo.

Tangu kamanda Khalifa Haftar alipoanzisha mashambulizi mapema mwezi huu kuudhibiti mji wa Tripoli, ambao hivi sasa uko mikononi mwa serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa. Katika taarifa yake ya awali, kupitia twita, shirika hilo lililaani mashambulizi dhidi ya wafanyakazi wa afya.Kutokana  na  mapigano hayo yaliyoanza Aprili 4 takribani watu 8000 wameyakimbia makazi yao nchini humo. Rais wa Misri Abdel-Fattha el-Sisi alikutana na Haftar mjini Cairo kufanya majadiliano juu ya mashambulizi huku kukiwa na shinikizo la kimataifa kukomesha mashambulizi hayo. Misri na Ufaransa zimeendeleza uhusiano na kamanda Haftar.


Tagi: WHO , libya , Mapigano

Habari Zinazohusiana