Watu zaidi ya 700 wameuawa  kutokana na dhoruba ya Idai Afrika Kusini

Dhuruba kali ya  Idai  yasababisha vifo vya watu  wasiopungua 700 nchini Msumbiki, Zimbabwe na Malawi

Watu zaidi ya 700 wameuawa  kutokana na dhoruba ya Idai Afrika Kusini

Watu wasiopungua 700 wameripotiwa  kufariki kufuatia dhaoruba kali iliotokea  nchini Msumbiji, Malawi  na Zimbabwe.

Mvua kali na upepo  iliosababisha  mafuriko nchini imepelekea maafa makubwa katika mataifa hayo  katika ukanda wa Afrika Kusini.

Waziri wa  mazingira wa Msumbiji Celso Correira amefahamisha kuwa watu 417 wamefariki kutokana na dhoruba kali hiyo ya Idai.

Watu waliofariki nchini Zimbabwe imefahamishwa kuwa watu 259 huku nchini Malawi ikitangazwa kuwa watu 56 pekee ndio waliofariki.

Shughuli za uokoaji bado zinaendelea  huku  mlipuko wa kipindupindu umeripotiwa katika ameneo yalioathirika na dhoruba hiyo ya Idai.

Watu zaidi ya  milioin 1 na nusu wakiwemo watoto wameathirika na dhoruba hiyo iliotokea wiki iliopita nchini Msumbiji, malawi na Zimbabwe.

Rais wa Msumbiji Filipi Nyusi alitangaza  siku tatu za maombolezo  nchini humo kufuati maafa yaliotokea kufuatia  dhoruba hiyo.Habari Zinazohusiana