Shirika la ndege la Ethiopian airline kufungua kesi

Shirika la ndege la Ethiopian airline kufungua kesi kutokana na kuchafuliwa na magazeti ya Marekani

Shirika la ndege la Ethiopian airline kufungua kesi

 

Shirika la ndege la Ethiopian airline kufungua kesi dhidi ya magazeti ya Marekani yaliyoandika habari za uongo kuhusiana na ajali ya ndege ya shirika hilo iliyosababisha vifo vya watu 157.

Kiongozi wa shirika hilo Tewolde Gebremariam, amesema magazeti ya Washington Post na New York Times yaliandika habari za uongo kwa ajili ya kuharibu mwonekano  wa shirika na nchi kwa ujumla.

Gabremariam alisema maandilizi yote kwa ajili ya kufungua kesi dhidi ya magazeti hayo yapo tayari.

Gebremariam, alisema habari hizo za uwongo zilizoandikwa na magazeti hayo zilikuwa na lengo la kusahaulisha watu kwamba Boeing 737 Max 8 ilipata ajali nyingine kabla ile ya ndege ya Ethiopian airline.

New York Times, iliandika kwamba rubani wa ndege  ya shirika hilo iliyopata ajali mwenye udhoefu wa masaa karibu elfu 8, Yared Getachew, hakuwa amepitia mafunzo ya kurusha ndege aina ya Boeing 737 Max 8.  

Washington Post kwa upande wao waliandika kwamba miaka mingi kabla hata ya ajali kulikuwa na malalamiko katika Idara ya anga ya Marekani kuhusiana uwezo mdogo marubani 2 katika kufuata taratibu za kiusalama.Habari Zinazohusiana