Uganda yamfukuza mkurugenzi mkuu wa MTN

Uganda yamfukuza mkurugenzi mkuu wa shirika kubwa la mawasiliano MTN kwa madai ya kutishia usalama wa taifa

Uganda yamfukuza  mkurugenzi mkuu wa MTN

Uganda wamtimua mkurugenzi mkuu wa shirika la mawasiliano la MTN nchini humo Wim Vanhelleputte, kwa madai ya kutishia usalama wa nchi hio.

Taarıfa kutoka polısi zinasema Mkurugenzi huyo alisafirishwa siku ya Alhamisi.

Barua iliysainiwa na waziri wa mambo ya ndani wa Uganda Jeje Odongo imeonyesha kwamba Wim Vanhelleputte hakubaliliki tena kuwepo nchini Uganda na akae mbali kabisa na nchi hio milele.

 

 


Tagi: MTN , Uganda

Habari Zinazohusiana