Mlipuko wa bomu waua wanafunzi wawili nchini Ethiopia

Wanafunzi wawili wameripotiwa kupoteza maisha baada ya bomu kulipuka karibu na shule moja nchini Ethiopia.

Mlipuko wa bomu waua wanafunzi wawili nchini Ethiopia

Wanafunzi wawili wameripotiwa kupoteza maisha baada ya bomu kulipuka karibu na shule moja nchini Ethiopia.

Kwa mujibu wa habari,bomu la kutegwa na mkono lilipuka karibu na shule moja katika mkoa wa Gondar eneo la Amhara,Kusini Mashariki mwa nchi hiyo.

Watoto wawili wamepoteza maisha huku wengine sita wakiwa wamejeruhiwa.

Enyewe Zewdie,msemaji wa polisi wa eneo hilo amesema kuwa uchunguzi unafanywa kufuatia mlipuko huo na ni vipi bomu lilitegwa karibu na shule.

Tagi: bomu , Ethiopia

Habari Zinazohusiana