Mvua kubwa yasababisha vifo vya watu watatu Sudan

Watu watatu wameripotiwa kupoteza maisha baada ya mvua kubwa kunyesha siku mbili mfululizo nchini Sudan.

1019302
Mvua kubwa yasababisha vifo vya watu watatu Sudan

Watu watatu wameripotiwa kupoteza maisha baada ya mvua kubwa kunyesha siku mbili mfululizo nchini Sudan.

Kulingana na kituo cha habari cha Sudan,watu wengine watatu hawajulikani walipo huku zaidi ya nyumba elfu mbili zimeangamizwa.

Kwa mujibu wa habari Kordofan ni eneo lililoathirika kwa kiasi kikubwa kutokana na  mvua hizo.

Waziri wa afya wa Sudan ametangaza kuwa huduma zote muhimu zimetumwa katika maeneo yaliyoathirika na mvua hizo.

Tagi: #Mvua , #vifo , #Sudan

Habari Zinazohusiana