Jean-Pierre Bemba anastahiki kushiriki kuwa mgombea katika uchaguzi mkuu JK Kongo

Chama cha ukombozi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo MLC chafahamisha kuwa Jean-Pierre Bemba, anastahiki kugombea kiti cha urais katika uchaguzi Disemba

Jean-Pierre Bemba anastahiki kushiriki kuwa mgombea katika uchaguzi mkuu JK Kongo

Chama cha ukombozi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo MLC chafahamisha kuwa Jean-Pierre Bemba, anastahiki kugombea kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa urais  unatarajiwa kufanyika  ifikapo Disemba 23 mwaka 2018.

Kwa mujibu wa chama hicho Jean-Pierre Bemba ambae kwa sasa umeachwa  huru na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita baada ya kukutwa hana hatia anastahiki  kushiriki katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Disemba 23.

Kiongozi wa zamani wa kivita  na naibu wa baraza la seneti huyo alikamatwa tangu  mwaka 2008 na kuhukumiwa adhabu ya kifungo cha miaka 18 akituhumiwa uhalifu wa kivita ulioendeshwa na wapiganaji wake kati ya Oktoba mwaka 2002 na Machi  mwaka 2003 Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita imemuacha Bemba huru kwa muda baada ya kutumikia kifungo miaka 10. Bemba   anaishi nchini Ubelgiji akiwa na familia yake akisubiri  hukumu ya mwisho.

 Habari Zinazohusiana