Watu 20 wajeruhiwa katika ajali ya ndege nchini Afrika Kusini

Watu 20 wajeruhiwa katika ajali ya ndege iliotokea  katika eneo la Wonderboom Kaskazini mwa jiji la Pretoria

Watu 20 wajeruhiwa katika ajali ya ndege nchini Afrika Kusini

Watu 20 wameripotiwa kujeruhiwa katika ajali ya ndege iliotokea  katika eneo la Wonderboom Kaskazini mwa jiji la Pretoria nchini Afrika Kusini.

Taarifa  kuhusu ajali hiyo imetolewa na kitengo cha kutoa huduma ya kwanza katika eneo la tukio.

 Kulingana na taarifa zilizotolewa na  msemaji wa  kitengo cha kutoa huduma ya kwanza zimefahamisha kuwa  watu wanne wamejeruhiwa  vikali huku wengine wakiwa na majeraha ya kawaida.

Picha zilizosambazwa katika mitandao ya kijamii zimeonesha  ndege iliokuwa na nemba ya Martin's Air Charter akiwaka moto.Habari Zinazohusiana