Mabalozi wa Afrika Umoja wa Mataifa wamtaka Trump kuomba radhi

Mabalozi 54 wa Afrika Umoja wa Mataifa wamtaka rais wa Marekani Donald Trump kuomba radhi baada ya matamshi yake ya kashfa

Mabalozi wa Afrika Umoja wa Mataifa wamtaka Trump kuomba radhi

 

Mabalozi 54 wa mataifa ya bara la Afrika Umoja wa Mataifa wamtaka rais wa Marekani Donald Trump kuomba radhi kufuatia matamshi yake ya kashfa yaliolenga mataifa ya Afrika na Amerika ya Kusini ikiwemo Haiti na El Salvador.

Mabalozi wa mataifa 54  ya Afrika Umoja wa Mataifa wamemtaka rais wa Marekani kuomba rdhi kwa mataishi yake ya kashfa dhidi ya Afrika.

Kutokana na jambo hilo balozi wa Marekani nchini Senegal na Botswana wameitwa na uongozi wa mataifa hayo kufafanua kuhusu matamshi hayo.

Matamshi hayo ya Trump yamechukuliwa kama matamshi ya ubazi wa rangi jambo ambalo lingestahili kukemewa na taifa kama Marekani.

Baada ya mkutano wa dharura wa mabalozi wa mataifa ya Afrika  Umoja wa Mataifa uliochukuwa muda wa masaa manne Ijumaa, Donald Trump ametakiwa kuomba radhi kwa mataishi yake machafu.Habari Zinazohusiana