Je wajua?

Je wamjua mwanamke mahiri katika masuala ya anga

Je wajua?

Dilhan Eryurt alihitimu kutoka  Chuo Kikuu cha Istanbul idara ya Hisabati na Utaalamu wa Astronomy.Mwaka 1959 alikwenda Canada kwa  kupata udhamini wa elimu na kusoma kwa miaka miwili . Kisha akaendelea kujifunza katika Taasisi ya Utafiti wa Goddard ya NASA, ambapo alipata ushirika kutoka Chuo cha Taifa cha Sayansi, ambako alisoma kuhusu jua.

 

Dilhan Eryurt, ambaye ametajwa katika historia kama mwanamke aliyeshinda katika masuala ya jua  alipewa "Tuzo ya Apollo ya Mafanikio ya NASA kwa watu wachache duniani kote kwa sababu ya michango yake katika mradi wa kutua Mwezini mwaka 1969.


Tagi: NASA , Uturuki

Habari Zinazohusiana