Leo katika historia

Matukio ya kihistoria ulimwenguni

Leo katika historia

1885

Mnamo tarehe 4 Januari 1885, upasuaji wa kidole tumbo wafanyika kwa mara ya kwanza, upasuaji huu ulifanywa na  Dr William West Grant  wa jimbo la Iowa nchini Marekani.Upasuaji huu ulifanywa katika mji wa Davenport.

 1967

Mnamo mwaka 1967  bomba la mafuta ghafi lenye urefu wa kilomita 490 lililoanzia kusini mashariki mwa Anatolia kuelekea ghuba ya İskender lilifunguliwa rasmi. Bomba hilo lililojengwa ili kusafirisha mafuta ghafi na lilijulikana kwa jina la bomba la mafuta ghafi la Batman-Iskender .

1969

Mnamo mwaka 1969 makubaliano ya kimataifa yaliyokuwa na lengo la kupiga vita aina yeyote ya ubaguzi wa rangi yalitiwa saini. Uturuki iliyathibitisha makubaliano hayo mnamo mwaka 2001.

 1976

Siku kama ya leo mnamo mwaka 1976  sanamu la farasi Trojan lenye urefu wa mita 12 lafunguliwa rasmi kwa ajili ya matembezi mjini Çanakkale. Farasi wa Trojan ni moja ya mada maarufu za filamu. Farasi huyu anafahimika vile alivyotumika kuwaficha askari ndani yake . Askari hao ndio waliowezesha kuuteka mji wa kale wa Troy uliopo Çanakkale.

 1986

Mnamo mwaka 1986 daraja la Fatih Sultan Mehmet linalounganisha bara la Ulaya na Asia lilianza kujengwa kwa mara ya pili.  

2010

Mnamo mwaka 2010, ujenzi wa Burj Khalifa, jengo linalojulikana kwa kuwa refu zaidi duniani ulikamilika. .Habari Zinazohusiana