Leo katika historia

Matukio ya kihistoria ulimwenguni

Leo katika historia

1870

Ujenzi wa daraja la Brooklyn,daraja lenye kutembelewa sana na watalii New York ulianza siku kama ya leo mwaka 1870.

1917

Siku kama ya leo mwaka 1917 wakati wa vita vya kwanza vya dunia waasi waliweza kutumia fursa ya kuanguka kwa uongozi wa Ottoman na kuwachoma moto waislamu 373 katika msikiti wa Ardahan.

1920

Mwaka 1920, Uturuki na Armenia zilifanya makubaliano ya amani.

1952

Mwaka wa 1952, watu 69 walikufa na watu 299 walijeruhiwa katika tetemeko la ardhi Erzurum na Hasankale.

1961

Press Ad Agency ilianzishwa kwa lengo la kuhakikisha kuwa kunakuwa na mgawanyo sawa wa matangazo ya magazeti mwaka 1961.

1976

Mwaka wa 1976, Agano la Kimataifa la Haki za Kijamii na Utamaduni lilianza kutumika. Uturuki ilisaini mkataba Agosti 15 mwaka 2000.

1990

Mwaka 1990, mchoro wa “wahamiaji” uliochorwa na mchoraji wa Kituruki  Ibrahim Balaban uliuzwa kwa milioni 45 ikiwa ni kiasi cha fedha kikubwa zaidi kulipwa kwa ajili ya mchoro katika zama hizo.

2004

Mwaka 2004, ndege ya Air Boeing 737  ya kampuni ya binafsi ya ndege nchini Misri iligonga bahari ya Shamu na kusababisha vifo vya watu 148.Habari Zinazohusiana