Mesut Özil, uraia na timu ya taifa ya kabumbu ya Ujerumani

Kutoka katika kitengo cha utafiti wa kisiasa, uchumi na jamii SETA, Can ACUN anatufafanulia

Mesut Özil, uraia  na timu ya taifa ya kabumbu ya Ujerumani

Barani Ulaya kunashuhudiwa kwa kiasi kikubwa  ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya uislamu.  Ubaguzi wa rangi, chuki dhidi ya uislamu inashuhudiwa baada ya sakata la mchezaji nyota wa kabumbu wa timu ya taifda ya Ujerumani mwenye asili ya Uturuki Mresut Özil. Tukio hilo nchini Ujerumani baada ya timu yake ya taifa kushindwa kuendelea katika michuano ya kombe la  dunia ni mfano ulio hai  unaoashiria  ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya uislamu..

 Kutoka katika kitengo cha utafiti wa kisiasa, uchumi na jamii SETA, Can ACUN anatufafanulia

      Mchezaji kabumbu wa timu ya taifa ya Ujerumani Mesut Özili amepiga picha akiwa pamoja na rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan na  baadae kuibua mjadala katika vyombo vya habari nchini Ujerumani. Vyombo vya habari nchini Ujerumani  vilichukulia kitendo hicha cha Özil kupiga picha tais Erdoğan kama kitendo kisichokuwa cha kawaida.  Kitendo hicho nchini humo kilizungumziwa  mno kabla ya michuano ya kombe la dunia kuanza.

Kştendo cha Özil kupiga picha na rais wa Uturuki kimechukuliwa kama kitendo kisichukuwa cha kawaida hadi kuzungumziwa na vyombo vya habari nchini Ujerumani na kupelekea matendo na matamshi ya chuki dhidi ya uislamu na ubaguzi kuongezeka nchini Ujerumani.

Mesut Özil ameshambuliwa kwa kashfa na  maneno ya kejeli  na vitisho.  Özil alikuwa mkimya kwa muda mrefu licha ya kukabiliwa na vitisho na maneno ya kashfa. Kiongozi  Reinhard Grindel  alizungumzia pia suala hilo na shirika la soka la Ujerumani.

Kushindwa kwa timu ya Ujerumani kuendelea katika michuano ya kombe la dunia na kuondolewa mapema katika michuano hiyo  tuhumu na lawama ametupiwa Mesut Özil. Jambo hilo  ni kama tonya la maji katika suala zima la ubaguzi na chuki dhidi uislamu.

Mesut  alitoka katika ukimya na  kutoa ujumbe katika ukurasa wake wa Twitter na kusema kuwa wakati timu ya Ujerumani inaposhinda basi yey huwa mjerumani na pindi inaposhinda basi moja kwa mowa mhamiaji. Hali hiyo inaonesha kuwa chuki dhidi ya uislamu na wageni imeongezeka nchini Ujerumani. Kulizungumziwa pia  Mohammed Ali.

 Kufautia hali hiyo imeonekana kuwa Mesut Özili  amekuwa mtetezi wa jamii ya wachache na  waturuki waislamu  wanaoishi nchini humo.

Rais Erdoğan amezungumzia pia suala hilo na ushindi ambao  uliokuwa ukipatikana kwa mchango wa Mesut Özil katika timu ya Ujerumani. 

Ni jambo la kushangaza  kuona  tukio kama hilo kutokea. Ubaguzi na chuki vinastahili kupigwa vşta na kukemewa. 

Hali hiyo iliotokea imepelekea  mwanasoka huyo kuwa kama msemaji wa waislamu na jamii ya waturuki nchini Ujerumani.  Kutokuwepo na wawakilishi katika bunge la Ujerumani  kumeonekana kuwa moja  ya matatizo  ambayo yanajitokeza dhidi ya wageni na  uislamu.

Ubaguzi na chuki dhidi ya uislamu  vinazidi kila kukicha  nchini Ujerumani.

 Habari Zinazohusiana