Hikaya za Anatolia

Hikaya za Anatolia,Kemer,Antalya

Hikaya za Anatolia

Leo katika hikaya za Anatolia tunawaleteeni kisa cha Chimera yani katika hadithi za zamani za Ugiriki,Chimera alikuwa ni mnyama aliyekuwa akitoa moto mdomoni.

Leo tutatizama sehemu muhimu kabisa wa utalii wa Antalya katika moja ya wilaya ijulikanayo kwa jina la Kemer.Kemer ni sehemu yenye kuvutia watalii wengi ambao hutembelea Antalya nchini Uturuki.

 

 

Ukiwa katika ufukwe wa bahari ukaelekea mbele kidogo kuelekea magharibi basi utakutana na sehemu hiyo ya Kemer.

Kemer inajulikana kwa mandhari nzuri ya kuvutia kwani unaweza kuiona bahari na baada ya pwani tu kuisha unaanza msitu mnene.Ukitembea kilomita 30 katika wilaya hiyo utakutana na moto ambao haujawahi kuzimika kwa miaka 30.Moto huo umehadithiwa katika hadithi za kale.Wakazi wa hapo huuita moto huo Chimera huku jina lake la kihistoria ni Khimaira.Katika lugha ya kigiriki Khimaira ilimaanisha farasi mwenye mabawa.Ukitizama katika unajimu angani,jina hilo linaaminika kuwa jina la mkusanyiko wa nyota mbalimbali mbinguni.

 

Tukitizama hadithi zilizohadithiwa na watu wa zamani wa Anatolia,hapo zamani za kale kulikuwa na farasi yenye mabawa.Farasi hiyo ilikuwa na mmiliki wake.Siku moja mmiliki huyo akaamua kuiuza farasi hiyo kutokana na hali mbaya ya kimaisha.Tajiri aliyeinunua farasi hiyo alishindwa kujua ni vipi ataitumia.Kutokana na kutokuwa na ujuzi kuhusu farasi huyo,tajiri huyo aliamua kuitumia kawaida katika kazi za shamba na kadhalika.Siku moja ghafla alitokea kijana mmoja na kuipanda farasi ile.Farasi ilimtizama kijana yule juu ya mgongo wake na ghafla ikaanza kupaa.Ilimzungusha kijana yule mawinguni,hewani,mbinguni na kisha ikarudi.

Kijana mwingine mahiri Bellerophontres kuona hivyo alitamani sana na yeye kuipanda farasi hiyo.

 

Alijaribu kuipanda lakini farasi iligoma kupaa.Bellorophontra akaambiwa kuwa endapo anataka kuipaisha farasi hiyo basi ni lazima atoe kafara katika hekalu ya Athena.Akifanya hivyo ombi lake litakubaliwa.

Kijana huyo alifanya kama alivyoelekezwa.Basi usiku alipolalala akamuona mungu Athena akimpa kipande cha dhahabu.Akamwambia kuwa atakuwa mmiliki mpya wa farasi hiyo kwa kutumia kipande hicho cha dhahabu.Toka siku hiyo kijana huyo alikuwa akiipanda farasi hiyo vile atakavyo na pia kupaa nayo kila mahala.

 

Siku moja kijana huyo aliipanda farasi hiyo na kuanza kufanya ziara sehemu tofauti.Moja ya sehemu aliposimama kijana huyo,mke wa mfalme wa mahala hapo alimpenda.Kijana yule akamkataa malkia yule na mwisho wake malkia akasambaza habari kijiji kizima kuwa kijana yule alikuwa akimtaka.Basi mfalme kusikia hivyo,roho haikumpa kumuua kijana mzuri kama yule na badala yake akaandika barua kwa mfalme wa Likya,Antalya na kumtuma nayo huyo kijana.Kijana akapeleka barua kama alivyoagizwa kwa mfalme wa Likya.Mfalme alimkaribisha kijana kwa furaha na kumhudumia kama mgeni kwa siku tisa.

 

Baada ya kufungua na kuisoma barua ile mfalme huyo alisikitishwa sana na kisa chote.Nae hakuwa na moyo wa kumuua kijana mzuri kama yule.Basi mfalme huyo hakuwa na jinsi,akaamua kumtuma kijana huyo katika safari ambayo alikuwa na uhakika asingeweza kurudi.Alimtuma akamuue mnyama wa ajabu msituni.Mnyama huyo kichwa kilikuwa cha simba,mwili wa mbuzi na mkia wa nyoka.Mnyama huyo alikuwa akitoa moto mdomoni.

 

Kijana yule akapanda farasi yake na kuelekea msituni.Alifanikiwa kumuua mnyama huyo kwa kurusha mkuki kutokea angani.

Baada ya mnyama huyo kufa,moto uliokuwa ukitoka mdomoni haujazimika mpaka wa hivi leo.Watalii wengi kutoka katika sehemu tofauti ulimwenguni huitembelea sehemu hiyo.

 

Siku hizi watu wanaamini kuwa endapo mwanamke asiyefanikiwa kupata watoto,akiuzunguka moto huo mara tatu basi hubarikiwa watoto.Mtu akipika nyama ya kulungu sehemu hiyo basi kila atakachoomba kinakubaliwa.

Kati ya watu maarufu waliotembelea sehemu hiyo ni Evliya Çelebidir.

 

Tukutane tena wiki lijalo kwa hikaya motomoto za Anatolia.Habari Zinazohusiana